Waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki
amewataka waandishi waabari wa kike kutumia kalamu zao katika kuandika mambo
yanayo hamasisha amani na utulivu nchini
Waziri huyo aliyasema hayo katika uzinduzi wa kikundi cha
HABARI GROUP, ambacho mlezi wake ni Naibu Waziri wa katiba na sheria Mhe.
Angella Kairuki ambaye aliahidi kuwa bega kwa bega na kikundi hicho
ilikuhakikisha kuwa kundi hilo linasonga mbele
Kagasheki alisema, Uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi ni moja
ya maadhimisho 12 ya ulingo wa Beling hivyo mnachofanya hapa ni katika
kujikwamua wenyewe kiuchumi na kama mnavyofahamu wanawake wanamajukumu mengi
katika familia, tasnia pia imewabana sana ila bado mmethubutu kufanya kazi,
endeleeni hivyo hivyo” Alisema
Aidha, Mratibu wa kikundi hichi Bi. Rabia Bakari amesema
kuwa kikundi hicho kinahitaji zaidi ya Sh.Millioni 10 ilikuwawezesha wanachama
wake kupata mikopo itakayo wanufaisha
“Kwa sasa katika akaunti yetu tumefanikiwa kuwa na million 2
nanusu tu, hivyo tunaitaji zaidi ya Milioni 23 ilikuweza kukopeshana na
kukamilisha malengo ya chama hicho” Alisema Rabia
Hatahivyo waliweka kukusanya zaidi ya sh. Millioni 6 katika uzinduzi huo, ambapo
mgeni rasmi alitoa Milioni 2.
EmoticonEmoticon