DANADANA ZAENDELEA, MATOKEO YA URAIS KENYA


Huku wakenya wengi wakiwa na shahuku kubwa ya kujua ninani kaibu kidedea katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo katika ngazi ya urais, danadana zimeendelea kuibuka juu ya matokeo hayo.

Uchaguzi mkuu wa Kenya ulimalizika kwa amani mnamo tarehe 4 mwezi wa machi huku kukiwa na utulivu mkubwa miongoni mwa wakenya

Aidha Kenya iliamua kutumia Teknologia mbayo ilikusudiwa kuepusha mizozo juu ya nani mshindi lakini jambo hilo lilifeli mpaka kufikia hatua ya kura kuesabiwa kwa mikono kama ilivyokuwa kwa siku za nyuma

Tayari baadhi ya wagombea wameonyesha kutokubaliana na matokeo yaawali ambayo yanaendelea kutangazwa, huku wachambuzi mbalimbali wakitangaza kutoiamini tume iliyopewa dhamana ya kusimamia zoezi zima la uesabuji kura

Hadi hivi sasa Bwana Uhuru Kenyatta anaongozi kwa kura Milioni mbili na laki saba huku Bwana Raila Odinga akina Kura Milioni mbili nalaki tano

Wakenya wameaswa kuwa watulivu huku wakisuburi matokeo hayo kutangazwa rasmi kama ilivyoahidiwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.
  


EmoticonEmoticon