Naibu Waziri wa
Elimu Mhe. Filipo Mulugo Asubuhi hii anatarajia kutangaza majina ya
wanafunzi walio chaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na wale
watakao jiunga na vyuo vya ualimu na ufundi
Majina yakupangiwa
shule pamoja na vyuo yamechelewa sana tofauti na ilivyo zoeleka,
kwani kwa taratibu za awali majina hayo hutangazwa mwezi wa tano
ikiwa ni miezi miwili kabla ya kufungua shule ili kutoa nafasi kwa
wazazi na wanafunzi kujiandaa na kujiunga na masomo yao
Katika hali isiyo
yakawaida majina hayo yata tangazwa hii leo ikiwa tayari shule
zimefunguliwa huku waliingia kidato cha sita wakianza masomo yao huku
kukiwa hakuna wanafunzi wa kidato cha sita
Endapo shule itakuwa
imefungua ikiwa na wanafunzi wa kidato cha tano basi pia itakuwa
maajabu mengi juu ya mfumo wa elimu, Ikumbukwe kwamba matokeo ya
wanafunzi hawa kwa mwaka 2012 yalitikisha nchi kutokana na asilimia
80 yawanafunzi kufeli vibaya huku idadi ya wanafunzi wachache ndio
walifaulu.
Kutokana na hali
hiyo Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda alilazimika kuunda
tume ya kuchunguza sasabu za kufeli kwa wanafunzi hao na baadae
ikapatikana pendekezo la kufanya standardization ili kuweza kuoka
idadi kubwa ya wanafunzi waliofeli na baadae matokeo kutangazwa upya
Hata hivyo baada ya
Standardization kufanyika ilitegemewa kuwa wizara itatoa taarifa ya
kutangaza ni wali na lini wanafunzi watajiunga na masomo yao ya
kidato cha tano kwa wale waliofaulu kwa vyuo na kidato cha nne
Habari zinazo husiana
Bonyeza hapa chini ili kusoma zaidi juu ya matokeo ya kidato cha nne 2012 tangu kutangazwa mpaka hii leo
Habari kamili itakujia hapa hapa .....................
1 comments:
Kwa muda uliobaki jamani tutajiandaaje hasa sisi wazazi na kama mtoto wako ulikwisha mpeleka shule inakuwaje??
EmoticonEmoticon