Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo.
1. Nauli za Daladala –
Jiji la Dar es Salaam
Umbali
wa Njia
|
Kiwango
Kipya cha Nauli
|
Mfano
wa Njia
|
Kilomita
kati ya 0 – 10 (Na mipaka ya Jiji Kati)
|
Sh
400/=
|
Ubungo
– Kivukoni
|
Kilomita
kati ya 11 – 15
|
Sh
450/=
|
Mwenge
– Temeke
|
Kilomita
kati ya 16 – 20
|
Sh
500/=
|
Tabata
Chang’ombe – Kivukoni
|
Kilomita
kati ya 21 – 25
|
Sh
600/=
|
Pugu
Kajiungeni – Kariakoo
|
Kilomita
kati ya 26 – 30
|
Sh
750/=
|
Kibamba
– Kariakoo
|
2. Nauli za Mabasi ya
Masafa Marefu
Daraja
la Basi
|
Nauli
ya zamani kwa km-abiria
|
Nauli
mpya kwa km-abiria
|
Mfano
wa kiwango kipya cha nauli kwa baadhi ya njia
|
|
Basi
la Kawaida kwa njia ya lami
|
Sh
30.67
|
Sh
36.89
|
DSM–Mbeya
Km 833
|
Sh
30,700
|
Basi
la Kawaida kwa njia ya vumbi
|
Sh
37.72
|
Sh
46.11
|
S/wanga-KigomaKm
551
|
Sh
25,400
|
Basi
la hadhi ya kati (Semi Luxury
|
Sh
45.53
|
Sh
53.22
|
DSM–Mwanza
Km 1,154
|
Sh
61,400
|
Mabasi
ya masafa marefu yaendayo mikoani
Nauli
za usafiri wa mabasi makubwa ya masafa marefu nauli hizo zimeongezeka
kwa viwango tofauti. Mathalani. Basi
la kawaida kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya ni Sh30,700, njia
ya vumbi kutoka Kigoma hadi Sumbawanga Sh25,400 na basi la
hadhi ya kati (Semi Luxury) kati ya Dar na Mwanza ni Sh61,400, wakati
basi la hadhi ya juu (Luxury) kati ya Dar na Arusha ni Sh
36,000.Kilima
alisema: “Kuanzia Aprili 12 mwaka huu, kati ya kilometa 0 hadi 10, nauli ya daladala itakuwa Sh400 badala ya Sh300 zinazolipwa hivi sasa.“Pia nauli za mabasi ya kwenda mikoani zimeongezeka kwa asilimia 20.3 kwa mabasi ya kawaida, mabasi ya kati kwa asilimia 16.9 na mabasi ya daraja la juu kwa asilimia 13.2,” alisema.
Kilima alisema nauli za - Mabasi ya mikoani zimepanda kutoka Sh30.67 hadi Sh36.89 kwa kilometa - Mabasi ya daraja la kawaida katika njia za lami. Kwa upande wa - Mabasi ya kawaida kwa njia ya vumbi imepanda kutoka Sh37.72 hadi Sh 46.11 kwa kilometa na kwamba - Mabasi ya hadhi ya kati, nauli zimepanda kutoka Sh45.53 hadi Sh 53.22 kwa kilometa.- Mabasi ya hadhi ya juu nauli zimepanda kutoka Sh51.64 hadi Sh58.47 kwa kilometa.“Kupanda kwa nauli kunatakiwa kwenda sambamba na huduma bora na kwamba Sumatra imepiga marufuku kutumia wapigadebe kuuza tiketi za safari”alisema.
Usafiri wa ReliKatika uamuzi huo, usafiri wa reli pia umepanda ambapo daraja la kwanza Dar es Salaam hadi Morogoro, nauli mpya na ya zamani katika mabano ni Sh21,100, (Sh16,852), Dar hadi Dodoma Sh34,700, (Sh27,788), Dar es Salaam-Tabora Sh54,800, (Sh43,859).Dar es Salaam-Isaka Sh62,100, (Sh49,662), Dar- Shinyanga Sh65,300 (Sh52,229) Dar –Mwanza Sh74,800 (Sh 59,818), Dar- Kigoma Sh75,700, (Sh60,599)
Daraja la pili,
Dar es Salaam-Morogoro Sh16,600, (Sh13,280), Dar es Salaam-Dodoma Sh26,400 (Sh 21,092), Dar es Salaam-Tabora Sh40,500 (Sh 32,364), Dar es Salaam-Isaka Sh45,800, (Sh36,605), Dar es Salaam-Shinyanga Sh48,000 (Sh38,390),Dar es Salaam- Mwanza Sh54,700 (Sh43,747), Dar es Salaam-Kigoma Sh55,400 (Sh44,305).
Daraja la tatu,
Dar es Salaam-Morogoro Sh8,800 (Sh6,138), Dar es Salaam-Dodoma Sh13,500 (Sh9,374), Dar es Salaam-Tabora 20,400 (Sh14,173), Dar es Salaam-Isaka Sh22,800 (Sh15,847), Dar es Salaam –Shinyanga Sh24,000 (Sh16,628), Dar es Salaam-Mwanza Sh27,200 (Sh18,860), Dar es Salaam- Kigoma Sh27,500 (Sh19,084).
Akizungumzia tozo za majini, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mamlaka hiyo imeridhia ongezeko la tozo la asilimia 34.3 kwa vyombo vinavyotumia bandari za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Alisema awali TPA walipendekeza tozo hizo kuongezeka kati ya asilimia saba hadi 400 kulingana na aina ya huduma zinazotolewa kwa meli zinazotumia bandari za mamlaka hiyo.
EmoticonEmoticon