Watu waliopanga nyumba za shirika la
Nyumba la taifa kiolela sasa kutimuliwa bila notisi endapo hawata
timiza mashariti waliopewa na shirika hilo ndani ya miezi mitatu
iliobaki
Akitoa taarifa hiyo kwa umma,
Mkurugenzi wa usimamizi wa rasilimali za shirika la Nuyumba Bwana
Hamad Abdala amesema, wametoa miezi mitatu iliwaweze kuhalalishwa
ukaaji wao kwani kukaidi agizo hili fursa yakutambuliwa haitakuwepo
tena.
Baada ya Fursa hii kupita nyumba hizo
zitapangishwa kwa watu wengine, kwani kukaa bila mkataba kwa sababu
yoyote ile inamaana makubaliano na masharti ya upangaji na shirika
hilo sio hahali. Alisema Abdala
Kama itapita mwezi mmoja bila kutimiza
masharti hayo, itachukuliwa kuwa ni ukiukaji wa mashrti ya upangaji
kwamaana hiyo shirika litalazimika kuwatoa kwani watakuwa wameonyesha
kuwa hawaitaji upangaji. Alisema Abdala
Hivi sasa mkataba wa upangaji
umebadilika nakuwa ya miaka mitatu nasiyo ya awali ambapo mpangaji
alikuwa akipanga moja kwa moja
Aidha mwaka 2010 shirika la nyumba
liliwatangazia watu wote waliopangishwa kwenye nyumba za shirika
kinyume cha taratibu kujitokeza iliwaweze kupewa upangaji lakini hali
hiyo imejirudia tena na kuilazimu shirika hilo kutoa miez mitatu kwa
wale wote waliopanga kiholela kutafuta upangaji wahalali
EmoticonEmoticon