AJALI YA JAHAZI NUNGWI - NAHODHA AKAMATWA

JESHI LA POLISI ZANZIBAR, limewataka wananchi kutoa tarifaa kama kuna ndugu au jamaa anaeofiwa kufa ndani ya ajali ya Jahazi iliyotokea siku ya ….. kwani hadi hivi sasa kuna majina ya watu 9 ambao hawajulikani walipo natarifa zinasema walikuwemo ndani ya Jahazi hiyo

Akiongea na Blog hii kwanjia ya simu, Inspector Mohamed Muhina Afisa habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, idadi ya watu waliodhaniwa kupanda kwenye Chombo hicho imeongezeka kutokea 32 hadi 37, tofauti na ilivyo dhaniwa baada ya Ajali kutokea.


“kama kuna mtu anajua ndugu yake alisafiri na chombo hicho kutoa tarifa iliwaweze kuhorodhesha kwenye orodha hiyo” Alisema

Chombo hicho ambacho kilisajiliwa kwaajili ya kubeba mizigo lakini ilibeba na abiri, tayari jeshi la polisi Zanzibar imeamu kuwachukulia hatua Nahodha wa chombo hicho bwana, Amekiba Salum na msaidizi wake ni Abdalah Salehe Kaji ilikuwaeleze ni kwanini wameamua kubeba abiria nasio mizigo

“Jeshi la polisi aliusiki na Udhibiti wa hivi vyombo ila tunawasiliana na mamlaka husika ilikuwea kuwachukulia hatua nahodha na msaidizi wake ambao mpaka sasa tunawashikilia” Alisema Inspector Muhina

Katika ajali hiyo iliyotokea taree moja, Watu ishirini na saba walinusurika kufa Jahazi lilokuwa likitokea Tanga kuja Unguja kuzama eneo la Mkondo wa bahari Nungwi

Jahazi hilo lilikuwa na jumla ya watu 37 pamoja na mizigo mbali mbali ndani yake ikiwemo  magunia ya bidhaa mbali mbali, chanzo kikihofiwa kuwa ni kuzidishwa kwa mizigo na idadi kubwa ya watu


EmoticonEmoticon