Shirika la umeme Tanesco limewatoa hofu
wanachi kwa kukanusha juu ya kuzimwa kwa mitambo ya Songas pamoja na
kukauka kwa bwala la Mtera, na kusisitiza kuwa hakuna mgao wa umeme
kwa sasa, hayo yamesemwa na Bi Badra Masoud ambaye ni msemaji wa
TANESCO
Pia Shirika hilo limewaomba radhi
Wananchi wanaofikwa na usumbufu pindi umeme unapo katika kwani
shirika hilo linadhamira ya dhati ya kutatua matatizo ya umeme
nchini. Alisema Badra
“Mitambo ya Songas haita zimwa, wala
Bwawa la Mtera halija kauka kiasi cha kuzima uzalishaji wa umeme
katika bwawa hilo japokuwa kiwango cha uzalishaji kimepungua kutoka
Megawati 80 mpaka Megawati 40 lakini aiwezi kufanya tukazima mitambo
hiyo, tutatumia kiwango cha umeme kinacho patikana na sio kuzima
mitambo hiyo” Alisema Bi Badra
Akifafanua zaidi juu ya swala la
Kampuni ya Songas kuzima mitambo yake Bi Bibadra amesema, Kampuni
hiyo tayari imepewa kiwango cha fedha ya Deni wanalo dai japo kuwa
hawajamali kulipa deni hilo. Hatahivyo Bi Badra alisikitishwa na
kitendo cha kampuni ya Songasi kusema kwenye vyombo vya habari kuwa
inaidai Tanesco na kuwa itazima mitambo yao ilhali njia za mazungumzo
kati yao inaendelea
“Sivyema kwa Songas kulalamika kwenye
vyombo vya habari, kama Tanesco wameshindwa kuelewana na sisi yupo
baba yetu mama yetu Wizara ya Nishati na Madini waende kule na
kulalamika na madai yao yatasikilizwa lakini tayari wamelipwa kiasi
fulani cha pesa” ...hakuweka wazi kiasi walicholipa.
AIDHA Tatizo lililopo hizi sasa ni
marekebisho ya miundombinu ambayo yanaendelea kote nchini kwani
kwamuda wa miaka 10 shirika hilo halikuwekeza kwenye miundombinu,
hali inayopelekea kuwepo kwa uchakavu wa Nguzo, Nyaya na miundombinu
muhimu. Alisema Bi Badra
“Hivi sasa marekebisho ya miundombinu
yanaendelea maeneo mbalimbali hali inayopelekea kukatika kwa umeme,
marekebisho yatachukua muda lakini tunaomba watanzania wawe
wavumilivu' hali hii itaisha, kikubwa nikuweka sawa miundombinu yetu”
Alisema
Sabubu ambazo Bi Badra aliziita kuwa ni
UN PLANED SHUT DOWN, nimiongoni mwa matatizo yanayopelekea umeme
kukatika baadhi ya maeneo akitolea mfano, kuibwa kwa nyaya za umeme,
kukatika kwa nguzo za umeme, wizi wa mafuta ya transfoma na mengine
mengi kama mvua kali au upepo mkali nimiongoni mwa mambo
yanayopelekea umeme kukatika.
Shirka la hilo linasikitishwa na
kukatoka kwa umeme hata kwa sekunde moja kwani hali iyo inapotokea
uinyima mapato shirika hilo na kuieleza jamii kuwa inania ya dhati ya
kuboresha matatizo yaliyopo hivi sasa, ilikuzuia matatizo ya kukatika
kwa umeme
Kwa zaidi ya mwezi sasa Umeme umekuwa
ukikatika katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam, na maeneo
mengine hali iliyopelekea wananchi kuhoji endapo kuna mgao wa umeme
lakini Tanesco wamekanusha kuwepo kwa Mgao licha ya umeme kukatwa
mara kwa mara
EmoticonEmoticon