Miongoni
mwa wanawake Elfu 6200 ambao hugundulika kuwa na Saratani, katiyao
wanawake Elfu 4300 ufariki kila mwaka kwa ugonjwa huo. Wengi wawana
wake hao niwenye umri kati ya miaka 15 na 44 ambao usumbuliwa na
Saratani shingo ya kizazi
Akiongea
le jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa mpango wa pamoja wenye
lengo la kudhibiti tatizo hilo, Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii
Mhe. Dkt Hussein Mwinyi amesema, Serikali pamoja na wadau wenye nia
ya kusaidia taifa watashirikiana juu ya ugonjwa huo
"Niwanawake Elfu 4300 ndio wanao fariki kutokana na saratani ya shingo ya kizazi kila mwaka, miongoni mwa wale Elfu 6200 ambao hugundulika kuwa na ugonjwa huo hapa nchini" Alisema Dkt Mwinyi
Aidha Waziri aliwataja Wadau
hao kuwa ni Chama cha Wazazi na Malezi (UMATI), Marie stopes
international pamoja na PSI, Ambao kwa pamoja wametangaza nia
yakuungana na serikali katika kudhibiti tatizo la kansa ya shingo ya
kizazi
Hatahivyo, Waziri amewataka wanawake na watu wengine kwa ujumla kujijengea tabia
ya kwenda kucheki Afya yao ilitatizo liweke kudhibitiwa mapema
Kwa
mujibu wa tafiti za Afya Duniani, hivi sasa ugonjwa wa Saratani
(Cancer) ndio ugonjwa unaoongoza kwa kuuwa watu wengi zaidi
ikifuatiwa na Maleria na Ukimwi
EmoticonEmoticon