SERIKALI kesho itatakiwa kutoa tamko Bungeni juu ya malalamiko ya Vitendo vinavyo tendwa na askari wa Kenya na Uganda wanaoingia nchini na kuwatesa Raia kwakile wanachodai nikutafuta wahalifu
Akitoa agizo hilo leo Bungeni, Mhe. Spika wa Bunge mama Anne Makinda amesema Serikali itatatiwa kuja kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo na hatua zitakazo chukuliwa juu ya malalamiko hayo.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Bungeni wa Ukerewe Mhe. Silvester Machemli kuwa, kuna askari wanchi hizo mbili wamekuwa wakitesa raia wa Tanzania kwa kuingia hadi nchini maeneo ya mipakani kwa kisingizio cha kutafuta wahalifu kisha kuwatesa na kuwapiga
"Naomba Bunge lijadili hili swala kwa usalama wa Nchi, kwani Askari wa Kenya na Uganda wanaingia nchini na wanawapiga na kuwatesa raia wetu kwakisingizio cha uhalifu" Alisema Silvester
Hatahivyo baada ya ombi hilo kutolewa Mhe. Spika alifunga mjadala kwa kutoa agizo la kuitaka Serikali kuja Bungeni hapo na kuelezea juu ya Tukio hilo la kuwepo kwa Askari wa Kenya na Uganda wanaotesa raia wa Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon