WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MHE. SHAMSHI VUAI NAHODHA |
AKIONGEA Bungeni hii leo Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamshi Vuai Nahodha amekanusha
kuwepo kwa majeshi ya nchi jirani ya Kenya na Uganda kuingia nchini
kinyemela na kutesa raia kama ambavyo iliwasilishwa Bungeni jana na
Mbunge wa Ukerewe Mhe. Silvester Machemli
Akijibu hoja hiyo leo Bungeni kama
ilivyo ahidiwa na Spika wa Bunge, Waziri wa ulinzi amesema kuwa
siokweli kuwa Askari hao wanawatesa raia ila kunamafunzo ambayo
yanaendelea eneo hilo la ukerewe baina ya nchi hizo na Tanzania
“Sikweli kwamba wanajeshi wa nchihizo
wanatesa raia na wameingia kinyemela ila kuna mafunzo yanaendelea ya
kudhibiti wavuvi haramu wanaotumia nyavu ndogo, na wanajeshi hao wako
nchini ambao ni kutoka Kenya, Uganda na Tanzania” Alisema Waziri
Aidha Waziri alisema, Mafunzo hayo
yanayoendelea yanatambulika na Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza, Ofisi
ya Kata na Kitongoji cha Ukerewe na kuwa siokweli kwamba taarifa ya
wanajeshi hao haijaifikia jeshi la polisi
Hatahivyo waziri wa Ulinzi alikemea
vikali kitendo cha Kiongozi kutoa taarifa bilaya kukifanyia uchunguzi
na ufahamu wa kina, nakumataka mtoa hoja angefanya utafiti kwanza na
sio kudanganya umma wawatanzania, Alisema
Naye mtoa hoja hiyo Mhe.Silvester
Machemli akikemea vikali kauli ya Waziri huyo ya kumuita kuwa ni
muongo na kwamba hajafanyia uchunguzi kile alichokisema huku
akisisitiza kuwa anaushahidi wakile alichokiwasilisha hiyo jana kuwa
wanajeshi wanchi hizo wananyanyasa raia huku akitaja majina ya
wananchi wa jimbo lake waliohadhirika na kadhia hiyo
WASANII/ WAFANYA BIASHARA WAPIGWA BITI
– SARE ZA JESHI
Leo Waziri wa Ulinzi ametoa kauli nzito
juu ya Wasanii na watu wanaofanya Biashara ya kuuza nguo ambazo
zinafanana na sare ya Jeshi la Polisi waache mara moja kwani atakaye
bainika Hatua kali za kisheria zitachukuliwa
Akijibu swali lililo ulizwa na Mariam
Msabaha Mbunge wa Viti Maalum, ambaye aliuliza serikali inawadhibiti
zipi watu wanaotumia sare za Jeshi kwenye uhalifu, Waziri ulinzi
amesema kwa wale wasanii wanaovaa sare zinazo fananana na zakijeshi
nimarufuku
“Kwa mtu yeyote asiye husika
kuendelea kutumia sare zinazofanana na zakijeshi, Tutaendelea
kuwasaka na hatutasita kuwachukulia hatua zakisheria kwa mujibu wa
sheria” Alisema Waziri wa Ulinzi
Aidha amewataka watu wanaofanya
biashara za nguo ambazo nisare za jeshi kuacha mara moja biashara
hiyo kwani siruhusa kwa mtu yeyote kumiliki sare hizo au kuuza
EmoticonEmoticon