VYUO VIKUU VYATAKIWA KUREKEBISHA KASORO ZAO KWA WAKATI
Tume ya vyuo vikuu
Tanzania TCU, imetoa wito kwa Wanafunzi na Menejmenti ya vyuo vyote nchini
kuchukua hatua kurekebisha kasoro mbalimbali zinazojitokeza vyuoni mwao kwa
wakati ilikudhibiti madhara yanayoweza kujitokeza
Wito huo umetolewa,
baada ya Tume hiyo kuingilia kati mgogoro ulidumu kwa wiki tatu katika chuo kikuu
cha kimataifa cha Kampala, na kubaini matatizo ya uongzi wa chuo hicho na
kuutaka uongozi wa chuo hicho kushugulikia matatizo hayo
Madai ya wanafunzi
hao nipamoja na, Ada na malipo mengine, kukosekana kwa kitabu cha matarajio(Prospectus),
Huduma za maktaba, Huduma za Intanet, Mfumo wa mitihani ya marudio, Sifa ya
utafiti na maandiko kwa wanafunzi wa mwaka wa tatu, Sifa ya walimu, Serikali ya
wanafunzi na katiba yake,Uwakilishi wa wanafunzi kwenye kamati na vyombo
mbalimbali vya chuo,
Malalamiko mengine
ni, Ufundishaji katika Shahada za udaktari wa binadamu na uhandii, Wanafunzi wa
Kitanzania kufikiriwa kulipa ada ya chini kuliko wageni, Ratiba za vipindi
pamoja waalimu kuwa na vipindi vingi,Kitengo cha Udhibiti wa ubora cha chuo(KIU
Quality Assurance Unit), mahafali na miadhara ya kielimu, Matokeo kutolewa kwa wakati
kupitia mtandao,.
Utaratibu wa
wanafunzi wenye sifa za Diploma kujiunga na Kozi mbalimbali za ngazi ya
Shahada,na malipo wakati wa kujiandikisha chuoni, ni maeneo ambayo yanaitajika
kutolewa ufumbuzi. na makubaliano yaliyofikiwa nikuwa matatizo yote yatatuliwe
EmoticonEmoticon