MANDELA BADO YUKO HOSIBITALINI KWA MATIBABU



Rais wa kwanza wa Afrika Kusini Nelson Mandela, anayetibiwa kwa kuugua ugonjwa wa mapafu, anaendelea vyema na matibabu

Bwana Mandela,mwenye umri wa miaka 94, alikimbizwa katika hospitali ya kijeshi, mjini Pretoria, siku ya Jumamosi.na hivi leo madaktari wanaomshugulikia wameelezea haliyake inavyozidi kuimarika
.
Hata hivyo Taarifa za bwana Mandela kuendelea kuwa hospitalini, zimezua wasiwasi nchini Afrika Kusini, tayari kuna tetesi za watu kutunga nyimbo za kumuenzi Raisi huyo wa zamani

Aidha Magonjwa ya mapafu yanaweza kusababishwa na virusi au viini tete. Pia yanaweza kusambazwa kupitia kwa kikohozi au kupiga chafya na yanaweza kuambukizwa kwa kugusa sehemu ambazo mgonjwa amegusa.

Kuna majina tofauti ya magonjwa ikizingatiwa sababu na sehemu ya mwili ambapo ugonjwa ule umeambukizwa.


EmoticonEmoticon