CHADEMA WALIA NAMCHAKATO WA MAONI YA KATIBA MPYA
Chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kimemtaka Rais akumbushwe kujibu barua ya Mwendelezo wa Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko M4C, ili itumike kushinikiza Serikali kuchukua hatua stahiki juu ya mambo mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Bw.Freeman Mbowe, amesema kuwa chama hicho kimechukua fursa hiyo kueleza baadhi ya masuala yaliyojiri kwenye mkutano wa kamati kuu ya chama hicho ambao ulifanyika kwa siku mbili ya taree 15 na 16, Dec 2012.
"Mazungumzo yaliyofanyika kati ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Rais Jakaya Kikwete, juu ya hoja ya kuundwa kwa Tume ya kimahakama kuchunguza mauaji na haja ya Rais kuchukua hatua na muendelezo wa M4C", ni muimu kuwa Raisi akumbushwe, alisema Mbowe
Mbowe amesema, tarifa ya hali ya siasa, Mapendekezo ya mwendelezo wa operasheni za vurugu la mabadiliko M4C, pamoja na mchakato wa mabadiliko ya katiba nimiongoni mwa vitu vilivyopewa kipaumbele
Aidha, Kamati hiyo imeitaka Tume ya mabadiliko ya katiba kuwasilisha mapendekezo ya Chadema juu ya katiba mpya na mapendekezo kwa serikali juu ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba awamu ya pili na tatu kwa pamoja, lengo nikupata katiba mpya na bora kwa taifa, alisema Mbowe
Kamati hiyo imeazimia, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kutoa mapendekezo ya kurekebisha katiba mpito kuhakikisha tume huru ya uchaguzi na marekebisho ya sheria zinazo simamia uchaguzi yanafanyika kabla ya katiba mpya, Alisema Mbowe
EmoticonEmoticon