LEMA KURUDI TENA BUNGENI, TUNDU LISU APONGEZA MAHAKAMA KUTOA UAMUZI HUO
Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania leo, imemrudishia ubunge Godless Lema aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliyo vuliwa na Mahakama kwa tuhuma ya kukiuka taratibu za Uchaguzi
Jopo la majaji watatu waliotoa hukumu hiyo, wakiongozwa na Jaji Natalia Kimaro, Wamesema kimsingi watu waliopinga Ubunge wa Bw.Lema hawakuwa na haki kisheria kufungua shauri hilo
Apiril mwaka Huu, Mahakama kuu kanda ya Arusha ilimvua Ubunge Bw. lema kufuatia kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa chama cha Mapinduzi CCM, Kwa madai kuwa Mhe. Lema alikiuka taratibu za uchaguzi ikiwa nipamoja na kutoa Lunga za kashfa didhi ya aliyekuwa mgombea kupitia CCM. Badilda Buriani
Aidha katika maelezo yake, wakili wa Mhe. Lema Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lisi amepongeza maamuzi ya Mahakama rufaa kwa kutoa hukumu ya haki
EmoticonEmoticon