SUKARI YA TANZANIA KUCHUNGUZWA NCHINI KENYA
Bodi ya sukari nchini Kenya (KSB) imeanza mchakato wa kuchunguza sukari kutoka nchini Tanzania na Uganda baada ya takwimu kuonyesha kwamba uingizaji wa sukari kutoka nchizi hizo mbili kuongezeka sana kwa miezi michache iliyopita
Mapema mwezi huu KSB iliyapiga makampuni mbalimbali ya Tanzania na Uganda kuingiza sukari nchini humo, Hatahivyo bodi hiyo ililegeza msimamo wake ilikupisha sikukuu za Christmas kupita, huku wakifanya uchunguzi wasiku chache na mamlaka za Tanzania na Uganda.
Kwa mujibu wa Jarida la Daily Nation la Kenya, Mkurugenzi wa bodi ya KSB Bi Rosemary M'kok amesema kwamba Bodi yake ina mamlaka ya kuchunguza ubora na uingizwaji holela wa sukari nchini humo, nakudai kuamini kuwa wafanyabiashara wa Kenya na Uganda wengi awana uaminifu
Kwamujibu wa takwimu, uingizaji wa sukari toka Uganda umeongezeka toka Tani 73 mpaka tani 30elfu kwa miezi 11 mwaka huu. Huku Tanzania ikiwa imesafirisha tani 504 kwa miezi 11 kuwenda nchini Kenya. alisema Bi. Rosemary
EmoticonEmoticon