WABUNGE WA UKRAINE WAZICHAPA BUNGENI
Wabunge wa Ukraine
wame zichapa Bungeni, katika kikao cha kwanza cha Bunge hilo, ambapo
walitakiwa kupiga kura ya kuidhinisha uteuzi wa Waziri mkuu mpya,
Mykola Azaron.
Habari
iliyochapishwa na mtandao wa www.Euronews.com, inasema kuwa Wabunge wa
Upinzane na wale Wabunge wa chama Tawala walijikuta kwenye hali ya
kupigana na kusukumana, baada ya wabunge wa upinzani kutaka kupiga
kura ya kumpinga Waziri huyo
Kwa upande mwingine
Wabunge wa Chama cha Upinzane walikuwa wakishutumiana, baada ya
wenzao wawili kugeukia upande wa serikali, kitendo ambacho kiliwaudhi
upinzania na kuzidisha zogo bungeni humo.
Chama tawala
kinaitwa Party of Regions, nakile cha upinzani kinaitwa
Batkivshchyna’, Lakini
hayo yakiwa yanaendelea Ndani ya Bunge baina ya Wabunge wa chama
tawala na kile cha upinzani
Kulikuwa na tukio jingine likiendelea nje ya Bunge Hilo.
Kundi
kubwa la watu 100 lilikuwa nje ya Bunge hilo kwa maandamano, ambao ni
wafuasi wa kundi la FEMEN ambao walikuwa wakijaribu kuingia ndani ya
Bunge hili kwa madai ya kuchoshwa na rushwa inayofanywa na viongozi
wao, na habari zinasema kuwa waandamanaji hao walikuwa nusu uchi
Hatahivyo hisio mara
ya kwanza kwa wabunge hao kupigana, Mwakajana walipiga baada ya
kutofautiana kwenye mabadiliko ya muswada
EmoticonEmoticon