DIAMOND AUKANA U FREEMASON, AWASHANGAA WANAOENEZA KUWA KABADILI DINI
Msanii anaye Ng'ara katika Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva hivi sasa, Diamond Plantum amekana kushiriki wala kujihusisha na imani inayousishwa na nguvu za giza ya "Freemason", na kusikitishwa sana na watu wanao sambaza maneno ya kuwa yeye amebadili dini.
"Mimi sijawahi kujiusisha na imani ya Freemason na wala sijui juu ya hilo kabisaa, Nimelelewa katika imani ya Kiislamu na ninacho juwa nikuwa Mungu ni mmoja....Siwezi Kuwa Freemason Hata siku moja"Alisema Diamond.
Akiongea na Campasvision Diamond, alisema Zaidi ameumizwa sana na kusikitishwa sana na habari zinazo zagaa kuwa yeye kabadili dini, kitu ambacho sio kweli..alisisitiza kuwa awezi kuiacha dini yake na kuwa na imani tofauti na aliyo lelelwa na kudai kuumizwa na watu wanao eneza habari hizo, Alisema Diamond
Vijana wanaoiga na Kukopi kazi zangu, kimsingi nafrahishwa sana tena inanipa nguvu yakuwa kazi zangu zinakubaliwa hata nawasanii wenzangu, Swala ambali linanifanya niongeze juhudi zaidi katika kuboresha kazi yangu. Alisema Diamond
Akiongelea juu ya Video Mpya ya Kesho Diamond alisema, amefurahishwa sana na Wimbo huo kwani ni miongoni mwa nyimbo ambazo Mashahiri yake hayakumpa shida kutunga kabisa kwa ilikuwa kama masihara lakini kilichotoka nikitu ambacho kimesimama. Alimalizia Diamond
EmoticonEmoticon