JOSEPH CHAMELEONE ANUSURIKA KIFO SIKU YA BOXING DAY 2012


Joseph Chamilione na mkewe Daniella
Msanii maarufu wa nchini Uganda Joseph Chameleone na mkewe Daniela, jana walinusurika kufa baada ya mtu mmoja kuvamia nyumba hiyo akiwa na Petroli kwa lengo la kumuua msanii huyo, lakini akiwa kwenye hazma ya kutekeleza tukio hilo moto wa Petroli aliotaka kuwachoma na ndani ya nyumba ya msanii huyo uli muunguza vibaya mtu aliyetaka kufanya tukio hilo

ALIYE JARIBU KUMUUA MSAANI WA UGANDA JOSEPH CHAMELEONE AFARIKI DUNIA

Mtu huyo aliye fariki masaa mawili yaliyo pita, Akipatiwa matibabu amefaamika kwa jina la Robert Kalamagi mwenye umri wa miaka 27, mkazi wa Seguku Kampala Uganda, amefikwa na umauti baada ya kujeruhiwa vibaya na moto wa petroli ambao alikuwa akijaribu kumwagia mke wa msanii huyo,

Daniela ambaye ni mke wa Chameleone, aliwaambia wa andishi wa Habari kuwa, Asubuhi ya Boxing Day alisikia vishindo sebuleni, wakati akiwa chumbani na alipojaribu kujua ninani, aligundua ni nani alimkuta marehemu na akajaribu kumuuliza anataka nini lakini akumjibu chochote, Alisema Daniela.

Aidha mke wa Msanii huyo alimuita Chameleone, ndipo mtu huyo alichukua geleni la lita tano kwa lengo la kumwagia Daniela, kinyume na matarajio yake petroli ilimwagikia yeye na alipo washa moto, aliungua kiasi cha kufanya mtu huyo kujeruhiwa vibaya na moto huo, Daniela anasema mtu huyo aliomba msaada alipokuwa anaungua na moto huo.

Kilicho washangaza watu wengi wa nchini Uganda ni baada ya mtuhumiwa kuwaeleza Polisi alipofanyiwa Mahojiano akiwa Hospitali kuwa, yeye ni shabiki mkubwa wa msanii huyo, na kilichotokea kwake alitumwa na mtu ilikumuua msanii huyo


Hatahivyo Polisi wa nchini humo wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kubaini kama hilo nitukio la ujambazi au alitumwa na mtu kutekeleza tukio hilo


EmoticonEmoticon