WEMA ALIOTENDEWA RAY C, WENGI WANAUHITAJI

DEAR PRESIDENT


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete Jana alitolewa na baadhi ya vyombo vya Habari akiwa na Msanii maarafu nchini Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, wakiwa ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Msanii huyo alienda kutoa shukrani zake baada ya Raisi kumpatia msaada wa Matibabu ya maradhi yanayo msumbua ya kuathirika na madawa ya kulevya (mpaka kufikia Kuwa teja).

Mimi ninamtizamo tofauti juu ya hili swala, na nisingependa kueleweka vibaya zaidi ya maoni yangu binafsi ambayo yanasumbua akili yangu. Ray C kweli anaitaji msaada lakini Maradhi aliyo pata niyasio epukika kwa mtu kama yeye?je akujua kuwa madawa yana madhara? sawa ni baati mbaya kama binadamu nilazima tusaidiene sina shida na hilo,kwani mama yake aliomba mwanaye asaidiwe kwenye vyombo vya habari

Maswali yangu yanakuja hapa,Nchi yetu aisapoti madawa ya kulevya tena kuna sera kali, Je huyu awekwe kwenye kundi gani? na ninajiuliza swali kama kweli Raisi ametoa msaada huo basi asiishie kwa Ray C, kwani kuna vijana wengi sana mtaani ambao wamejikuta wanaadhirika na madawa ya kulevya bila kupenda tena wakiwa na umri mdogo ambao wanafanya hayo bila kuamua wenyewe. Mpango huu uwafikie na wasioweza kufika ikulu na kuonana na raisi ambao ndio kundi kubwa la watu.research zipo kila Wizara na Taasisi ambazo zinashugulikia makundi haya ya watu ambao na wanaitaji msaada kama huu


EmoticonEmoticon