DIAMOND - SIWEZI KUMROGA TANZANITE
Star wa Bongo Fleva, Diamond Platinum, amefunguka juu ya sakata linalo endelea kati yake na msanii mwenzake Tanzanite, baada ya Tanzanite kusema kuwa anarogwa na Diamond, kiasi cha kuwa na maradhi yasiyo eleweka.

Akiongea na CampasVision Diamond amesema, Awezi kumroga Tanzanite "Nimroge iliiweje wakati nimemzidi vitu vingi sana, kama ni kuroga basi ninge waroga wale wenye mafanikio kimuziki na sio Tanzanite, hana kitu ambacho naweza kujifunza kutoka kwake, istoshe na mzidi kwa vitu vingi sana" alisema Diamond

Diamond alisema, malipo huwa ni hapahapa Duniani, yanayo mtokea yeye nimambo aliyo nifanyia mimi lakini mimi sijamfanyia chochote, pengine ni maradhi yake tu Mungu alipanga aumwe, sasa kutokana na  mambo yake binafsi anaisi ni mimi, aliongeza kuwa mimi nimtu wa Mungu sana siwezi kumfanya chochote" Alisema Diamond

Sasa hivi anaomba msamaa kwenye vyombo vya Habari, wakati alifanya watu wakanilaumu na kuniona mbaya kuwa nimeiba wimbo wake, kitu ambacho anajua siyo kweli, Mimi nimemsamee sana wala sina kinyongo naye, alisema Diamond

Hatahivyo, Tanzanite alisema anahisi kurogwa na Diamond kwani anaumwa maradhi yasiyo eleweka, kwani Diamond alimwambia atamfanyia kitu ambacho awezi kusaau maishani mwake , Nakumuomba sana Msamaa msani Diamond iliaweze kupona maradhi yanayo msumbua.


Pichani ni Tanzanite anaye dai kurogwa
" Namuomba Diamond msamaa sana, alisema sitasahau atakacho nifanyia, nandio sababu naamini pengine ni yeye atakuwa anahusika na maradhi yasiyo eleweka yanayo nisumbua, anisamee tu" alisema Tanzanite



EmoticonEmoticon