ASILIMI 80% YA WAKAZI JIJINI NAIROBI KUKOSA MAWASILIANO DECEMBER 31

Huku serikali ya Tanzania ikiwa kimya juu ya watu wangapi watakao athiriwa na zoezi la kuzimwa kwa mfumo wa Analogia  pindi ifikapo Decembar 31, ambapo kila TV zinapaswa kuwa na mfumo mpya wa Digitali, Tayari nchi jirani ya Kenya imetoa takwimu za watu watakao adhirika na zoezi hilo kwa jiji la Nairobi
Kwa mujibu wa habari za nchini humo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano wa nchi hiyo Dr. Bitange Ndemo, amesema zaidi ya asilimia 80% ya wakazi wa Jiji la Nairobi wataathirika pindi mitambo ya Analogia itakapozimwa.

 Habari zinasema, tayari vituo vya Television 20 zinarusha matangazo bure kwa wananchi, huku chanel zingine 40 zitalipiwa na wananchi ilikupata matangazo yao katika siku za karibuni. 

Waziri huyo amesema, zaidi ya wauzaji wa TV 150,000  jijini Nairobi, tayari wameingiza Ving'amuzi ambavyo zitawawezesha wananchi wenye TV za Analogia kuweza kupata mawasiliano kupitia TV za Analogia


EmoticonEmoticon