WADAU WALALAMIKIA TANESCO, NA MPANGO WA KUPANDISHA BEI ZA UMEME IFIKAPO MWAKANI
Wadau mbalimbali wameipinga ombi la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuongeza bei ya Nishati hiyo kwa asilimia 155 ifikapo Januari mwakani.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa pamoja, wadau mbalimbali walisema Tanesco aina sababu ya kupandisha bei ya umeme kwani bado inaweza kutumia rasilimali zake kujiendesha.
Aidha, Tanesco imeomba ipandishe bei ya umeme kuanzia mwakani kutokana na sababu kadhaa ikiwemo ongezeko la gharama za uendeshaji na kukithiri kwa madeni ya shirika hilo
Jumla ya Asilimia 81.7% ndio garama ambayo itaiwezesha Tanesco kuzalisha umeme bila kupata faida, kutokana na bei iliyopo hivi sasa.Alisema Mkurugenzi Mkuu wa Felchesmi Mramba.
Mramba alisema, hadi Oktoba mwaka huu,Tanesco ilikuwa inadaiwa kiasi cha Dola za Marekani 250 Milioni sawa na Sh.400 Bilioni, madeni hayo ndio huchangia kurudisha maendeleo ya shirika hilo.
Hatahivyo, Mramba alitaja madeni ambayo Tanesco inawadai wateja wake kuwa nikiasi kikubwa ambacho kinaweza kufidia hasara ambayo shirika hilo linapata.
Naye Mbunge wa Ubungo,ambaye ni Waziri kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini, alitoa orodha ya mafisadi wanayo ihujumu shirika la Umeme Tanesco, kuwa ni
1. Mhandishi William Geofrey Mhando,
2. Bw. Harun Mattambo,
3. Bw Robert Shemhilu,
4. France Mchalange na Naftari Kisanga na Sophia Msidai,
5. Mhandisi Declain Mhaiki na Bw. Suke, 6.Mhandisi D.Mhaiki, S.Nkondola, N.Ntimba.Mhandisi Cheger, Makia na Mwita. 7.Fatuma Chungu, Athanasius Nangali,Elangwa Mgeni
8. Lusekelo Kassanga (Mkurugenzi wa Fedha)
EmoticonEmoticon