KILIO CHA WANAFUNZI WA KIU CHAIFIKIA SERIKALI,
Kilio cha wanafunzi wa cho kikuu cha
kimataifa cha Kampala (KIU), Kimeifikia serikali baada ya Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu na Bunge. Willium Lukuvi kuonana
na baadhi ya Wanafunzi wa chuo hicho, leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam walikofikisha malalamiko yao
Willium Lukuvi amewataka wanafunzi hao
kutulia, kwani muafaka wa matatizo yao unafanyiwa kazi na kuwaambia kwamba ufumbuzi wake utajulikana Wiki
ijayo, Akiwataka Wanafunzi hao kutulia nakusubiri ufumbuzi huo
Kwa mudamrefu sasa, Wanafunzi wa Chuo
cha Kiu,wamekuwa kwenye mgomo baridi na maandamano ya hapa na pale
ilikutaka kupewa Mkopo kama wanafunzi wa vyuo vingine, juu ya ongezeko kubwa
la Ada pamoja kujua hadhi na uhalali wa chuo hicho kama kinaruhusiwa
katika ngazi ya Elimu ya Juu hapa Nchini
Hatahivyo Nchini Kenya, Mwezi mmoja
uliopita Taarifa ya Wizara ya Elimu ya Nchi hiyo ilitoa Tamko la kutotambua vyeti vya waitimu wa ngazi ya shahada ya chuo cha Kampla (KIU) Kilichopo nchini humo, licha ya
chuo hicho kuwepo takriban miaka kumi nchini humo kikitoa Elimu na mafunzo mbalimbali.
Baadhi ya Wazazi walitoa maoni yao nakutaka kujua uhalali wa chuo hicho kutokana na wasiwasi juu ya sakata hilo.
EmoticonEmoticon