ZAIDI YA MIAKA 20-25 TANZANIA KUPATA MEDALI KWENYE MICHUANO YA OLYMPIC
Filbert Bayi, alipokuwa akiongea na Campus Vision leo |
Kutokana na kutokuwepo kwa mfumo mzuri
wa michezo mashuleni Itaigarimu Tanzania miaka 20 mpaka 25, kupata
timu bora itakayo iwakilisha katika michuoano ya Olympic kulingana na
jitihada zilizopo hivi sasa
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Kamati
ya Olympic Tanzania (T.O.C) bwana Filbert Bay akiongea na Campas
Vision hii leo jijini Dar es Salaam, Bayi ambaye ameshinda tena
kitihicho kwa awamu nyingine, amesema Michezo mashuleni ndio itakayo
leta matokeo mazuri ya michezo nchini
“Kutokana na kuvurugika kwa michezo
ya Umitashumta, Sekondari kwa takriban miaka 15 hivi sasa, na kwa
jitihada zinazo chukuliwa hivi sasa miaka 20-25 ndio tutafanikiwa
kupata timu itakayo iwakilisha Tanzania Vizuri katika michuano ya
Olympic”Alisema Bayi
Bayi alisema, Ni muhimu kugawana jukumu
la kuinua michezo miongoni mwa wadau wote, ambao ni Mashuleni,Vyama
vya Michezo na Wachezaji ikiwa ni pamoja na Serikali kwa ujumla,
nakuwataka watu wanao laumu bila kutoa mchango wowote kutofanya hivyo
“Nirahisi sana watu kutoa lawama
pindi timu inaposhindwa, lakini hakuna anaye toa mchango na kujitolea
kuwasaidia katika mambo mbalimbali ambayo nayo yanakwamisha na
kupelekea kutopata Medali au kutofika mbali kimichezo”. Alisema
Bayi
Hatahivyo Bayi alitoa wito kwa Serikali
kuzisapoti shule binafsi zinazoonyesha uwezo wa kuinua michezo na
kuwataka baadhi ya Viongozi kuacha kuzirudisha nyuma na kuzipondea
shule hizo, kwani mfumo mzuri wa Michezo utapatikana kwa kukazania
michezo mashuleni
EmoticonEmoticon