Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr.Emanuel Nchimbi amewataka wanao miliki silahaa kinyume cha sheria kusalimisha haraka iwezekanavyo, kabla sheria kali azijachukuliwa didhi yao

Amri hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam baada ya kuwepo na kuzagaa kwa matumizi holela ya silaha ambazo zinatumika isivyo alali jambo ambalo linachochea uhalifu seemu mbalimbali nchini

Aidha Waziri Nchimbi amesema, Agizo la zoezi hilo lifanyike katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia taree 5 mwezi huu wa Dec, hadi taree 4 January mwakani, nakuongeza kuwa mara baada ya muda huo kumalizika oparesheni kali itafanyika nchi nzima.

Hata hivyo Nchimbi Amesema, watakao salimisha silaha kwa hiari yao wenyewe hatua za kisheria hazitakuchuliwa, bali watakao kaidi agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa didhi yao


EmoticonEmoticon