KAULI ZA MAGUFULI YAZIDI KUPIGIWA KELELE
Chama cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, kimeitaka serikali kufafanua
kauli aliyoitoa waziri wa ujenzi, Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli,
alipoalikwa kwenye mkutano wa kampeni za chama cha ODM
cha nchini Kenya kama ni ya serikali au yake mwenyewe.
Waziri kivuli wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Mbunge wa
Nyamagana mhe. Hezekiah Wenje, amesema hayo leo kufuatia kile alichodai
kuwa nihatua ya Tanzania kuingilia siasa za ndani za Kenya.
Wenje ameongezea kuwa endapo matatizo yatatokea kauli ya Mheshimiwa
huyo itakuwa imeleta tafsiri mbaya miongoni mwa wakenya
Kwa mujibu wa Wenje, chama hicho kimepokea malalamiko mengi kutoka
kwa Watanzaniawanaoishi Kenya kuwa huenda wakapata matatizo
endapo kutatokea kutoelewana baina ya pande hasimu
katika siasa za nchi hiyo hasa kipindi hiki nchi hiyo inapoelekea
kwenye uchaguzi mkuu.
nikukumbushe mpenzi msomaji juu ya habari hiyo
ambayo pia iliandikwa the blog hii ya Campas Vision
taree 7.12.2012
MAGUFULI NA KAMPENI ZA KENYA, ATUA NAIROBI KUMUUNGA MKONO RAILA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA NCHINI HUMO
Waziriwa Miundombinu Mhe. John Pombe Magufuli leo yuko Nchini Kenya ambapo amehudhuria kampeni za uchaguzi zinazo endelea jijini Nairobi, Akiwa anatoa sapoti kwa Waziri Mkuu wa Nchi hiyo Mhe. Raila Odinga anaye gombe nafasi ya Urais Raila Odinga ambaye ameungana na mwana siasa maarufu Kalonzo Musioka nakuanzisha chama chama cha OrangeNDC, ilikukabiliana na Wahasimu wao Uhuru Kenyata naWilium Ruto ambao nao wameungana, uchaguzi Mkuu wa Kenya unatabiriwa kuwa na Upinzani mkubwa kutokana na mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo Aidha, Uchaguzi utafanyika ifikapo March mwakani. huku kukiwa na kesi kwa baadhi ya Viongozi ambao wanagombea nafasi ya Urais, katika mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC . baadhi ya Tweets za leo za Viongozi hao
Kama unavyo onekana ni tweet za viongozi hao, pia Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai ameudhuria kampeni hizo
updates.
Magufuli asema, Raila anahofu ya Mungu na anafaa kuiongoza Kenya nakuweka msisitizo wa wananchi wa nchi hiyo kumpigia kura kiongozi huyo
EmoticonEmoticon