BAR 248 ZINAZO PATIKANA ENEO LA SINZA AZINA VYUMBA VYA KUIFADHI WALIOLEWA KUPINDUKIA

Barabara ya Shekilango mpaka Bamaga, eneo la Sinza, imebainika kuwa na Bar zinazo fika 250, baada ya mtandao wa kuzuia matumizi mabaya ya Pombe (Tanzania Network Against Alcohol- TANETS) kufanya utafiti katika kata 18 za jiji la Dar es Salaam.

Utafiti huo ulifanywa kwa muda wa wiki tatu, na miongoni mwa kata hizo ni Tandale, Mabibo, Mwenge, Kawe, Manzese, Ubungo, na Shekilango, umebaini kuwa eneo la Sinza ndilo linaloongoza kuwa na Bar nyingi zaidi, huku kukiwa na usalama mdogo wa kuwaifadhi waliolewa kupindukia

Tarifa hiyo imetolewa na Katibu Muoenezi wa TANETS, bwana Mathias Kimario, baada ya taasisi hiyo kutaka kujua juu ya kuzagaa na unywaji holela wa pombe katika jiji la Dar es Salaam

Bwana, Mathias alisema, miongoni mwa bar zote 250 zilizo fanyiwa utafiti katika eneo la Sinza bara bara ya Shekilango mpaka Bamaga, ni Bar Mbili tu Ndio zina vyumba maalumu kwaajili ya kuifadhi watu waliolewa kupindukia, na zilizo baki Walevi hutolewa nje bila kusaidiwa mahali pa kupumzikia 

" Bar mbili tu ndio zina vyumba maalum kwa ajili ya walevi kupindukia na kuwajali wateja wao wanapokuwa awajitambui kwaajili ya Pombe yani, 'Responsible Beverage Services', lakini zilizo baki azina huduma hiyo kitu ambacho uhatarisha maisha ya yule aliye lewa" alisema Mathias

Mwanamke anatakiwa kunywa pombe mbili tu, kutokana na kuwa na mafuta mengi mwilini, na kwa wanaume ni pombe 3 tu, kwakuwa wana maji mengi mwilini hivyo uwezo wakuchuja pombe ni mkubwa kuliko wanawake wenye mafuta mengi,  Alisema Mathias kutokana na tafiti mbalimbali zlizo fanywa nchi za Marekani.

Alisema, Kiwango cha watumiaji wa Pombe ni kikubwa sana, kwani utafiti unaonyesha watu 90 ambao wanatumia Pombe kila siku hunywa pombe zaidi ya 5 mpaka 6, kiwango ambacho nikikubwa sana na kusisitiza Watanzania kuacha kutumia Pombe kali. Alisema Mathias

Nivyema watu wakanywa Pombe maenoe ya nyumbani hasa katika siku za sikukuu na kusisitiza kuwa kutumia Pombe kali ni maswala yanayo ondoa usalama wa mtumiaji, kama ataendesha uku amelewa. Alisema Mathias


EmoticonEmoticon