WATANZANIA WATAKIWA KURIPOTI MATATIZO YA EAC
Watanzania
wametakiwa kuitaarifu serikali juu ya kero na unyanyasaji
wanaofanyiwa wanapoingia katika nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki kufanya biashara, ili serikali iweze kuchukua hatua.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, Dkt
Stagomena Taxi, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati
akizungumzia maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa wakuu wa nchi
wanachama wa jumuiya hiyo ulioisha hivi karibuni.
Bi.
Taxi amesema kumekuwa na malalamiko kadhaa ya wanayofanyiwa
Watanzania hususani jumuiya ya wafanyabiashara, na kwamba ni jumuku
la wafanyabiashara hao kuweka wazi kero hizo ili serikali iwasiliane
na nchi husika kwa lengo la kuzitatua.
Katika
mkutano huo, Mradi wa ujenzi wa bandari ya Dar es Salaam ulipewa
kipaumbele. Ilikuongeza kina cha gati no.1-7, ujenzi wa gati mpya
no.13 na 14, ikiwa nipamoja na matengenezo ya bandari za maziwa makuu
ya Victoria, Tanganyika na Bandari ya Kivu. Suala hilo litaiwezesha
Tanzania kufaidika kibiashara.
EmoticonEmoticon