SHULE NA VYUO KUFUNGWA HUADHIRI UKUSANYAJI WA DAMU SALAMA



Watanzania wameombwa kuendelea kuchangia damu kwa hiari hasa katika kipindi hichi cha mwezi Nov mpaja January kutokana na shule na vyuo vingi kufungwa kwani wachangiaji wengi wa damu ni wanafunzi ambao watakuwa likizo kwa miezi hiyo.


Wanafunzi wa vyuoni pamoja na wale wa shule za sekondari ndio wamekuwa wakijitolea kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji wa damu salama hivyo muda wa likizo idadi ya upatikanaji wa damu salama hupungua.

Akiongea na wanahabari katika ofisi zao jijini Dar es salaam, wakati akitoa taarifa ya ukusanywaji wa damu salama kwa kipindi cha Julai na sept mwaka huu Afisa Uhusiano wa mpango wa taifa wa damu salama bwana Rajabu Mwenda amesema wameweza kuvuka malengo na kukusanya asilimia 110 ya damu.


“Katika kipindi cha miezi 3 jumla ya chupa 38,552 zilikusanywa na kuvuka malengo ya chupa 35,000 zilizokuwa zinakusanywa katika vipindi vya nyuma nakufikia asilimia 110 kiasi ambacho nikizuri kwa matumizi ya damu hapa nchini” alisema Rajabu.


Aidha kanda iliyo ongoza kwa makusanyo ya damu ni kanda ya mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es salaam, Morogoro,Dodoma na Pwani ambapo jumla ya chupa 13,669 zilikusanywa. Kanda inayofuata kwa ukusanyaji damu ni kanda ya kaskazini ambapo ilikusanywa chupa 6,159 katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga.


Watanzania watakiwa kutambua kuwa Kuchangia damu mara kwa mara hupunguza magonjwa ya moyo, kurekebisha madini ya chuma mwilini, hivyo kusisitiza taasisi za kidini, wanafunzi makampuni pamoja na kambi za jeshi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wanaohitaji damu.


EmoticonEmoticon