Shirika la umeme nchini Tanzania
Tanesco limetangaza kuwepo kwa umeme wa mgao kuanzia tarehe16 mpaka
26 mwezi huu kutokana na upungufu wa gesi katika kisiwa cha
songosongo kilichopo wilayani Kilwa kuwa na matengenezo ya kiufundi
Shirika hilo linategemea kisiwa hicho
kupata gesi ya kuzalishia umeme ambapo vituo vya kuzalisha umeme kama
Ubungo, IPTL na nyingine zinazo zalisha umeme kwa kiwango kikubwa
zitaadhiriwa na ukosefu huo hivyo kupelekea kuwepo kwa mgao huo
Akiongea katika ukumbi wa idara ya
habari maelezo jijini Dar es salaam, msemaji wa shirika hilo bi Badra
Masoud amesema matengenezo hayo ni muhimu na haya kwepeki hivyo ndani
ya siku 10 kuanzia kesho mgao wa umeme utaanza.
“Mgao huu utakuwa wa muda si kwamba
umeme hautakuwepo kabisaa, kama mnavyo jua hivi sasa tumepunguza
uzalishaji wa vyanzo vya maji kutokana na mabadiliko ya Tabia nchini
na tunategema sana Gesi hivyo tutakosa gesi kutoka songosngo”
Alisema Badra.
Kutokana na matengenezo hayo mikoa
iliyo unganishwa katika gridi ya taifa ndiyo itaadhirika kwa kukosa
umeme, mikoa hiyo ni Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Tanga,
Kilimanjaro, Dodoma, Pwani, Singida, Tabora, Manyara, Mara, Morogoro
pamoja na Zanzibar.
Mikoa ambayo aitaadhirika na mgao huo
niile ambayo haijaunganishwa kwenye gridi ya taifa nayo ni Ruvuma,
Rukwa, Mtwara na Lindi.
Siku chache tu Bi Badra akiwa
kikaangano live kupitia ukursa wa facebook w a kituo cha utangazaji
EATV Bi. Badra alisema hakuta kuwa na mgao wa umeme nakuwa kilicho
kuwa kina endeleo mpaka kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo ni
matengenezo madogo madogo yaliyo kuwa yakifanywa na shirika hilo
Katika kipindi hicho bi Bandra alisema
watanzania hawataki maneno yakuwa umeme upo na badala yake wanataka
umeme nakuhidi kuwa shirika hilo litawapa huduma ya umeme
Hata hivyo uongozi wa Tanesco unaomba
radhi kwa usumbufu utaokao jitokeza kwa baadhi ya maeneo yatakayo
kosa umeme
Ikumbukwe kuwa shirika hilo limetuma
maoni yake ya kupandisha bei za umeme ifikapo mwakani licha ya kutoa
huduma isiyo ridhisha kwa wateja wake.
EmoticonEmoticon