Poulsen aunda kikosi kuikabili Harambee Stars


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16 kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.

Wachezaji walioitwa ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).

Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).

Viungo washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).

Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa SugarMbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC



 


EmoticonEmoticon