Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amepewa siku 7 ili kutoa hadharani ripoti ya tume ya aliyounda kuchunguza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 ambapo takribani asilimia 60 ya watahiniwa walifeli mitihani hiyo
Kauli hiyo imetolewa na mtandao wa wanafunzi nchini TSNP pamoja na jumuiya ya kuetetea haki za binadamu kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam UDHRA walipokuwa wakiongea na wanahabari hii leo jijini Dar es salaam
Akiongea kwa niaba ya wenzake mkurugenzi wa TSNP bwana Alphonce Lusako akitoa tamko hilo amesema wana sikitishwa na usiri wa tume ya uchunguza matokeo hayo tangu Machi mwaka huu majibu hayaja wekwa hadharani.
“Majibu yawekwe hadharani ili waliohusika na ufaulu mbovu wachukuliwe hatua kali kwa kudidimiza elimu ya Tanzania, hivyo Waziri mkuu ndani ya wiki moja atoe ripoti hadharani” amesema Alphonce
Aidha, amesema wanaitaka tume hisika iliyoongozwa na Profesa Mchome aliye kuwa katibu mtendaji wa taasisi ya vyuo vikuu TCU ambaye kwa sasa amepandishwa cheo nakuwa katibu mkuu wa wizara ya elimu ajitokeze atoe ripoti hiyo hadharani, amesema Alphonce
Wanafunzi hao pia walisiki tishwa na mkanganyiko uliojitokeza hivi karibuni juu ya uwepo wa division 0 na division 5 kati ya katibu mkuu wa wizara ya elimu Prof. Mchome na naibu Waziri wa elimu Mhe. Phillipo Mlugo.
Wizara ya elimu inapaswa kujikita kuondokana na umahututi wa mfumo wa elimu ndani ya taifa letu na kuweka mfumo bora wa elimu utaowatoa watanzania katika giza nene walilo nalo na kuwafundiosha stadi za maisha lakini wizara ya elimu imejikita kwenye divishen tu jambo ambalo ni hatari sana
Matokeo ya kidato cha nne mwaka jana watahiniwa 60.6% walipata sifuri, huku 5.16% ndio walifaulu nawengine 26.2% walipata daraja la nne, hata hivyo jumuiha hizi za wanafunzi zimewataka watanzania wote kujadili sana elimu kwani ndio msakabali wa taifa na maendeleo yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon