Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari hapa nchini na ikulu ya Tanzania
inasema Tanzania itatoa kikosi kimoja (Battalion
Group) na nchi nyingine ambazo zimekubali
kuchangia askari ama polisi
Katika Kikosi hicho ni Afrika Kusini,
Uganda, Algeria na Chad. Nchi
hizo zilijitokeza kushiriki katika Kikosi hicho wakati wa Mkutano wa
Wakuu wa Majeshi wa nchi hizo huko Pretoria, Afrika Kusini,
Mkutano
ambao maamuzi yake yameidhinishwa na kukubaliwa na wakuu wa nchi
akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete.
ACIRC
kitakuwa kikosi cha muda wakati Afrika
inaendelea na maandalizi yake ya kuunda Jeshi la Kudumu la Afrika
(Africa Standby Force)
na Lenye Uwezo wa Kukabiliana na Migogoro Haraka na Popote barani
humu (Rapid Deployment Force).
Jeshi
hili litakuwa ni jeshi lenye uwezo wa kuingia nchi yoyote, chini ya
AU, na hivyo wakati
mwingine litatumika kutuliza migogoro katika nchi yoyote ya Afrika
hata kama nchi husika haijaomba msaada wa jeshi hilo.
Jeshi
hilo litakalofanya kazi yake chini ya mfumo wa Amani na Usalama
katika Afrika – African Peace and Security
Architecture (APSA) litaiwezesha AU
kuwa na jeshi la askari na polisi wenye uwezo na nguvu kukabiliana na
mizozo ya kijeshi barani humo na kuwa vifaa vyake vitatolewa nchi
wanachama wa AU ambao watakuwa tayari kushiriki katika mpango huo.
EmoticonEmoticon