Watanzania wanao jihusisha na biashara ya usafirishaji wametakiwa kuchangamkia kiasi cha Pound Milioni 100 kilichotolewa na serikali ya Uingereza ambayo ni sawa na shilingi Bilioni 2.6 za kitanzania ili kuwasaidia katika kupata mitaji na kuendesha biashara zao
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Dr. Charles Tizeba wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kusaidia wachukuzi kupunguza garama za kusafirisha mizigo katika ukanda wa afrika mashariki mkutano uliohudhuriwa na Balozi wa Uingereza, na ziongozi wa jumuhiya ya Afrika mashariki
“Kiasi hichi cha fedha kitatumika katika kuendeleza miradi ya kitechnologia ambayo itatumika katika shuguli za usafirishaji na fedha zingine zita wawezesha wafanyabiashara katika ukanda wa Afrika mashariki hivyo watanzania wachangamke wasibaki nyuma feda hizo kukuzia mitaji yao.alisema
Hivi sasa Serikali ya Tanzania inajipanga kupunguza matatizo yasiyo ya kiforodha kwa wafanya biashara wanao vuka mipaka, kupunguza maeneo ya mizani pamoja na kuwakusanya wadau wote wakodi katika eneo moja ili kuwapunguzia wasafirishaji vizuizi zisivyo vya lazima hali ambayo itaongeza kasi ya kibiashara na masoko katika ukanda wa afrika mashariki.
MIGOGORO JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, BARAZA LA MAWAZIRI LA NCHI
WANACHAMA KUKAA NOV 30 KUJADILI
Wakuu wa nchi wanachama wa jumuhiya ya Afrika mashariki watakutana mara baada ya baraza la mawaziri wa nchi hizo kuukaa Nov. 30 mwaka huu kwa lengo la kujadili juu ya mgogoro uliopo katika jumuhiya hiyo.
Wakiongea katika uzinduzi wa mkutano wa jinsi ya kupunguza garama za kusafirisha mizigo kwa nchi wanachama wa Afrika mashariki Naibu waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki Dr, Abdalla Juma na Naibu Katibu mkuu wa jumuhiya hiyo Dr. Ennos Bukuku wamesema wananchi watulie kwani muafaka wa jambo hilo utajulikana baada ya kikao hicho.
“Unapofanya vikao pembeni ya jumuiya huku vikao hivyo vikihusu maendeleo ya jumuhiya hiyo bila kuwashirikisha nchi wanachama inakuwa aieleweki lakini tutakaa Nov. 30 mwaka huu kujua nini mstakabali wa suala hilo” Alisema Dr. Ennos Bukuku
Aidha aliwataka waandishi wa habari kuacha kufuatilia sana suala hilo na kutaka ufafanuzi wa mara kwa mara kwani kwa kufanya hivyo kwa weza kuvunja uhusiano uliopo hivyo wasubiri matokeo ya kikao hicho ambapo viongozi wa kuu wa nchi hizo nao watahusishwa. Alisema
Kwa muda sasa kumekuwa na hali ya sinto fahamu kwa wananchi wa jumuiya ya Afrika mashariki kutokana na mvutano uliyopo ambao unatishia muungano wa jumuhiya hiyo huku baadhi ya nchi wananchama wakiandaa mkakati wa kujitoa katika jumuhiya hiyo.
EmoticonEmoticon