KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI KIGOMA HAKIHUSIANI NA HABARI YA KIJANA ALIYE LIWA NYAMA YA USO WAKE


Taarifa ambazo thecampasvision imepokea hizi punde zinasema kifo cha  mwanahabari Issa Ngumba hazihusiani na habari aliyoiripoti November 24 mwaka jana ambayo ilimhusu kijana aliyeliwa nyama ya uso na Bosi wake huko mkoani Kigoma

Taarifa hiyo ambayo nimepokea kutoka mahali alipokuwa akifanyia kazi marehemu, kuwa miongoni mwa tarifa za kusisimua alizo ripoti marehemu kwa mara ya mwisho nipamoja na kijana aliye liwa nyama ya uso wake, Lakini si kweli kuwa ndio habari ya mwisho aliyo ripoti kwa mara ya mwisho

Tarifa hiyo imewaomba watu pamoja na wanahabari wasipotoshe ukweli wa Kifo chake kuwa kina husiana na Habari hiyo, kitu ambacho kitavuruga uchunguzi unaoendelea hivi sasa juu ya mauaji ya mwandishi huyo

Habari zinasema kuwa, Aliye kula nyama ya mfanyakazi wake bwana Imani Paul tayari alisha kamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria, yuko mahabusu na kesi yake inaendelea katika mahakama ya wilaya ya Kibondo mkoni humo

Aidha yule kijana aliyeliwa nyama ya uso wake hadi kupofuka macho kabisa ambaye alifahamika kwa jina moja tu la Susuruka anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Kibondo mkoani humo

Kumekuwa na taarifa mbalimbali zinazo sambazwa kuwa kifo cha marehemu huwenda kina husiana na tarifa aliyo ripoti ya kijana aliye liwa nyama ya uso wake na bosi wake ambaye alikuwa akimchungia ng'ombe kitu ambacho sio kweli na hakihusiani na mauaji ya mwandishi huyo

Tungependa kupata uchunguzi sahihi juu ya Tukio la Mauji ya mwandishi huyu. Marehemu Issa Ngumba (45) aliuwawa kwa kunyongwa huko kigoma na kisha kupigwa risasi mkononi huku Bastola na Simu zake mbili zikiachwa eneo la tukio. Ngumba alikuwa mtangazaji wa kituo cha Radio Kwizera ambayo inapatikana mkoani Kigoma

Jeshi la Polisi limeahidi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ilikubaini aliye usika na mauaji hayo pamoja na mmiliki wa Bastola ambayo ilitumika katika mauaji hayo





EmoticonEmoticon