Lulu akiwa anatoka Mahakama ya Kisutu chini ya ulinzi wa Askari Magereza. Picha na Loyce Joseph |
MAHAKAMA Kuu kanda ya Dar es Salaam imebadilisha siku ya kusilizwa kwa maombi ya dhamana ya Mwigizaji nyota wa filamu nchini, Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la Lulu,kutoka Ijumaa ya kesho hadi Juma tatu ya January 28 mwaka huu, na Kiasi cha Milioni 20 kinaitajika ili kuweza kuwekewa dhamana hiyo
Lulu anashtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa msanii mwenzake wa fani hiyo, Steven Kanumba, bila kukusudia.
Taarifa za ndani kutoka Mahakamani hapo zilizolifikia Blo hii na kudhibitishwa na vyanzo vya ndani kutoka Mahakamani hiyo zimedai kwamba msanii huyo anaweza kupata dhamana hiyo na kurudi uraiani huku akipangia tarehe nyingine ya kuwasilini Mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo.
Awali Lulu alikuwa akikabiliwa na kosa la kuua kwa kukusudia, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini baada ya upelelezi kukamilika alibadilishiwa mashtaka na kuwa ya kuua bila kukusudia, kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakakama Kuu.
EmoticonEmoticon