Joseph Mayanja maarufu kama Chameleone na mkewe Daniella Atim pamoja na Crew yake ya Leon Island, Huwenda wakafunguliwa mashitaka ya mauaji na Polisi nchini Uganda baada ya Kifo cha kijana wa miaka 27 Robert Karamagi
Hatua hiyo imekuja baada ya maelezo ya awali ya Familia ya Mwanamuziki Chameleone waliyatoa siku ya tukio la kuvamiwa ambayo ilikuwa ni boxing day mwaka jana kutofautiana na yale ambayo walitoa mashuhuda wengine ambao nao walishuhudia tukio hilo.
Shirika la Habari la nchini Uganga liliripoti tukio ambalo, Blog hii pia iliripoti. Siku ya Boxing day kuwa mwanamuziki huyo alivamiwa na kijana mmoja ambaye sasa ni marehemu,baada ya kuingia ndani ya Nyumba ya msanii huyo kwa lengo la kuwadhuru lakini baati mbaya alijijeruhi mwenyewe kwa kujimwagia Petroli kisha kujilipua kwa moto.
Kijana huyo alifariki siku moja baadae, alipofikishwa Hospitali kwa matibabu zaidi, Lakini Baada ya kifo cha kijana huyo Baba mzazi wa kijana huyo alijitokeza na kusema mwanae kauwawa na familiya ya msanii huyo na kuwa akujilipua mwenyewe kama ilivyodaiwa na Familiya ya Msanii huyo
Baba wa kijana huyo aliongeza kuwa kijana wake anaupungufu wa akili na kuwa msanii huyo alikuwa akifahamu
Picha ikionyesha matukio ya kijana huyo akiwa kwa msanii chameleone |
Habari zilizo chapishwa na tovuti ya SUNDAY VISION, zimetoa maelezo ya polisi kuwa. Watamfungulia mashitaka Msanii huyo kutokana na Maelezo yaliyotolewa na mashuhuda wa Tukio hilo,
Afisa wa Polisi Ibrahim Saiga amesema, wanaushahidi wa mhojiano ambayo yatatumika na kutumwa kwa Mkurugenzi wa mashitaka wa nchini (DPP). Tayari msanii huyo ameshatoa maelezo yake kwa polisi juu ya tukio hilo na ambavyo alijihusisha na tukio hilo
EmoticonEmoticon