SERIKALI ya Tanzania imekosa mfumo wa uhakika wa kushugulikia malalamiko ya matukio ya ukiukwaji wa Haki za binadamu hapa nchini, Mtandao wa watetezi wa Haki za binadamu nchini waeleza
Raisi wa Jumuhiya ya Wanasheria
Tanganyika, ambaye pia ni mwanachama wa Mtandao huo. Wakili Francis Stolla
amesema kumekuwa hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa pale ambapo mashirika
na asasi za kulinda haki za binadamu zinapopiga kelele juu ya swala hilo
“Kumekuwa na mauaji mbalimbali
yanayo laaniwa na kugusa hisia za watu, tena zinazotumia nguvu kama Risasi
lakini sheria za uundwaji wa Tume ambazo zinaundwa na serikali, wakati huohuo
serikali ndio inatuhumiwa, aifanyi haki kutekelezwa” Alisema Wakili Francis
Uundwaji wa Tume umekuwa sio
mzuri, ucheleweshwaji wa kuchukua hatua mpaka wananchi wana lalamika, kwani
wahusika hawafikishwi mahakamani hata pale tume inapopeleka Ripoti na Uchunguzi
wake kwa serikali lakini hatua madhubuti hazichukuliwi. Alisema Francis
“Kunachombo ambacho akiegamii upande wowote ambacho ni
KORONA, chombo hiki kipochini ya Mahakama kwani mahakama ndio imepewa mamlaka
ya kutenda haki pale Serikali inapokuwa kwenye mgogoro na Wananchi wake, kitu
ambacho nacho hakifanyiwi kazi vizuri” Alisema Francis
Hatahivyo Wakili huyo amesema, Hatawale wanaotetea haki za
binadamu nchini nao wanaitaji kulindwa kisheria ilikuwa na usalama wa maisha
yao. Alisema Wakili Francis
EmoticonEmoticon