SAJUKI KUZIKWA DAR, MAKABURI YA KISUTU, BONGO MOVIE WAMLILIA

PICHA IKIMUONYESHA WASTARA AKIBEMBELEZWA NA WAOMBOLEZAJI JANA KATIKA MSIBA WA SAJUKI HUKO TABATA BIMA (picha na Jackson Odoyo-habarimpya.com)



Marehemu Juma Kilowoko maarufu kama SAJUKI, atazikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam, baada ya mwili wake kufanyiwa dua. Sajuki amefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Tarifa kutoka kwa madaktari inasema, Marehemu alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya Ngozi, ugonjwa ambao umemsumbua kwa mudamrefu mpaka kufikwa na umauti.

Sajuki ambaye ameacha mke ambaye alikuiwa msanii mwenzake na ambaye wameshirikiana katika Movie nyingi, Wastara Juma na mtoto mmoja mwenye umri wa miezi tisa. 


Mahojianao ambayo CAMPASVISION iliyafanya na baadhi ya wasanii ambao hawakupenda majina yao yatajwe, Walisema ni heri Mungu ampumzishe sajuki kutokana na mateso aliyokuwa akiyapata kwa muda wa miaka miwili tangu alipobainika kuwa na maradhi ya kansa.

"Wengi tuampenda sajuki lakini kwa haya mateso bora Mungu ampumzishe, tutamkosa daima lakini kazi zake zitatufanya kuwa pamoja" walisema wasanii hao.

Hatahivyo Raisi wa Shirikisho la Filamu nchini TAFF Simon Mwakifwamba aliwaambia wandishi wa Habari kuwa, Wamefanikiwa kuishawishi familia ya marehemu ili aweze kuzikwa hapa jijini Dar es Salaam badale ya Songea kama ilivyo tangazwa hapo awali,

"Sajuki atazikwa Ijumaa katika makaburi ya kisutu, muda ni saa tano asubuhi wapenzi na watanzania ambao watapenda kutuunga mkono waje makaburi ya Kisutu"Alisema Mwakifwamba

Msiba upo eneo la Tabata Bima, ambako waombolezaji wamekusanyika ilikushirikiana na ndungu wa familia ya marehemu


EmoticonEmoticon