BREAKING NEWSSSSSSSSSSSSSS

VURUGU TENA MTWARA- KITUO CHA POLISI CHA VAMIWA, MWANDISHI WA KITUO CHA CHANEL TEN AJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO


Habari zakuaminika  zilizo rushwa na kituo cha Television cha EATV kipindi cha Hotmix hivi sasa, zinasema Kumetokea tena vurugu Mkoani Mtwara, ambapo kituo cha Polisi kimechomwa moto pamoja na Mwaandishi wa Habari wa Chanel Ten amejeruhiwa katika Vurugu hizo hata hivyo aikuelezwa kama kuna mtu amepoteza maoisha katika tukio hilo

UP DATES

Habari zaidi kutoka kwa mashuhuda huko Mtwara, Uharibifu ni mkubwa sana kwani IKULU ndogo imevamiwa na nyumba ya Mbunge Hawa Gasia imevamiwa. JWTZ na Mahakama pia zimevamiwa na inasemekana pia zimechomwa moto huku Polisi nao wakiendelea kupiga mabomu kuwatawanya wananchi hao

Chanzo cha Habari kinasema, Vurugu hizo zimetokana na Imani za Kishirikina pamaja na Askari Jeshi aliye waita wenzake na kuvamia wananchi baada ya kupigwa.

Mwandishi wa Chanel Ten aliye jeruhiwa ni JOHN KASEMBE na tayari amefikishwa Hospitali kwa matibabu zaidi

Habari zaidi utaendelea kujuzwa juu ya Habari hii 


EmoticonEmoticon