WATU 11 wameuwawa leo asubuhi na wengine kujeruhiwa vibaya katika eneo la Kibusu Tana river nchini Kenya katika Visa vya kulipiza kisasi kati ya jamii ya wa pokomo na jamii ya Orman. Na kupelekea idadi ya watu waliokufa tangu juzi kufikia 21
Watu kutoka jamii ya Orman leo majira ya
saa moja asubuhi wamevamia vijiji vya Pokomo na kuuwa watu 11, kwa
nia ya kulipa kisasi juu ya wenzao 10 waliyo uwawa jana asubuhi na
jamii ya Pokomo hata HotMix pia ilikujuza juu ya habari hiyo
Kiongozi wa kikabila wa eneo hilo Chief
Amuma Mkala na Babuya Komora ambaye ni Diwani wa eneo hilo kwa pamoja
walithibitisha kutokea kwa tukio hilo,
Shirika la Msalaba mwekundu nchini Kenya
limesema kuwa, miongoni mwa walio uwawa ni watoto watano, wanawake
watatu na wanaume watatu kutoka jamii ya Pokomo
Hatahivyo, Licha ya Raisi wa Kenya Mwai
Kibaki kutuma Askari 2, 000 katika eneo hilo bado mauaji yameendelea
kutokea, na mahofisa wa Polisi wanahofia kutokea mauaji mengine zaidi
December 21 mwaka jana watu 42 waliuwawa
katika eneo hilo na kupelekea idadi ya vifo vya wenyewe kwa wenyewe
kuongezeka hadi 160 tangu mwzi wa nane mwaka jana.
EmoticonEmoticon