WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII MHE. |
WIZARA
ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti
Ukimwi NACP, imetenga fungu maalum kwaajili ya kununulia Dawa za
kudhibiti magonjwa nyemelezi ya ugonjwa huo ilikukabiliana na uhaba
wa Dawa na Vifaa tiba katika vituo vyote vya umma
Akiongea
leo Bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.
Magreth Mkanga, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dr Hussein Mwinyi amesema Serikali
itahakikisha kuwa dawa hizo zinapatikana kwa wingi katika vituo vya
Afya ili kudhibiti uhaba wa Dawa hizo za magonjwa nyemelezi
Aidha
Dawa kama za Kifua kikuu, Kisonono na Malaria zinapatikana Bure Bila
malipo kwa watu wenye Virusi vya Ukimwi katika vituo vyote vya
kutolea huduma za Afya za umma na baadhi ya vituo Binafsi ambavyo
vimeidhinishwa na Wizara hiyo
EmoticonEmoticon