MWIGULU AWAFUNGULIA MLANGO WA NEEMA WANAFUNZI ELIMU YA JUU

MUSWADA WA MAREKEBISHO YA MFUMO WA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NCHINI UMEPITISHWA HII LEO  ILIKUWEZA KUFANYIWA MAREKEBISHO .Habari zaidi

Mhe. Mwigulu Nchemba akiongea Bungeni siku za nyuma   

Mbunge wa Iramba Magaribi na Naibu katibu mkuu wa CCM- Bara, Mhe. Mwigulu Nchemba leo amewasilisha hoja binafsi yakuiomba serikali kukubali kuleta muswada wa marekebisho ya sheria ya mfuko wa Elimu ya juu (Higher Education Fund) ilkutatua matatizo ya muda mrefu ambayo hulalamikiwa juu ya mfuko huo

Akiongea Bungeni, Mhe. Mwigulu amesema endapo Serikali itakubali kufanya marekebisho, itaipunguzia mzigo wa kugarimia Elimu ya juu katika Bajeti yake (Serikali) kwani hata Wizara zitagaramia helimu ya juu, kuliko mfumo uliopo sasa ambao umekuwa na malalamiko mengi wa kutenga bajeti kwaajili ya shuguli hiyo

"Tukiweka mfumo wa kila wizara kugarimia helimu ya juu kupitia fedha zake za matumizi Mengineyo kwa asilimia 80%, itasaidia Serikali kupata kiwango cha 100% kwakila mwanafunzi, kwani itawezesha kutobagua niyupi apewe mkopo na yupi asipewe" Alisema Mwigulu

Aidha, Alieleza kuwa mfumo ambao unamlazimu mwanafunzi anaye taka mkopo kusomea fani asiyo ipenda iliapate mkopo sio mzuri, kwani wengi husoma fani wasizozipenda. Alisema Mwigulu

Hatahivyo Hoja hiyo binafsi ilipitishwa kwa kishindo na Wabunge wote ambayo ilielezea Sababu za kwanini Serikali ilete mswada wa marekebisho ya sheria hiyo Bungeni


EmoticonEmoticon