Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na wakazi wa Mtwara hapo Jana |
Habari nilizo pata toka mtwara muda simrefu
KUPITIA,
kikao kilicho kaa kwa siku mbili mfululizo katiya Wajumbe mbalimbali
wanao wakilisha wanachi wa Mtwara na WAZIRI Mkuu, Hatimaye Gesi
Kubaki Mtwara na itazalishwa eneo la Madimba huku kiwango kidogo cha
Gesi kikisafirishwa kuja Dar, lakini Mtwara ndipo kutakuwa na Gridi
kubwa ambayo ita zalisha Megawati 600 za umeme.
Mawaziri
6, hii leo wametua mkoani Mtwara kumuunga mkono Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, kwaajili ya Kuongea na wakazi wa Mtwara juu ya mgogoro wa
mbola la Gesi kutoka Mtwara kuja Dares salaam. Mgogoro uliodumu kwa
wiki mbili sasa
Mawaziri
hao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi (Dkt. John P. Magufuli),
Waziri wa Uchukuzi (Dkt. Harrison Mwakyembe), Waziri wa Viwanda na
Biashara (Abdallah Kigoda), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Uwezeshaji na Uwekezaji, - (Dkt. Mary Nagu) na Waziri wa Elimu (Dkt.
Shukuru Kawambwa).
Wajumbe
wengi katika kikao hicho wamekataa swala la Bomba la Gesi kutoletwa
Dar es salaa, Miongoni mwa mambo yaliyo ibuka katika kikao hicho,
nipamoja na baadhi ya wajumbe kumkataa Mkuu wa Mkoa na kumwambia
Waziri mkuu aondoke naye
Moja kati ya Mitambo ya kuzalishia Gesi huko Mtwara |
Mengine
ni pamoja na kauli ya Hawa Gasia, ya kutoa kauli za uongo kuusu
MtwaraVijijini kuunga mkono suala la Gesi kwenda Dar huku Madiwani wa
Mtwara nao wakidai hawakuusishwa juu ya swala hilo.
Kikao
kinafanyika chini ya ulinzi mkali wa FFU, JWTZ na UWT (Usalama wa
Taifa). Wananchi wa Mtwara na maneo ya Lindi wamekuwa na mgogoro wa
wiki mbili juu ya Mbomba la Gesi kusafirishwa kuja Dar.
EmoticonEmoticon