IDADI ya vijana wanaojiunga na mafunzo ya
elimu ya juu nchini Tanzania imeongezeka na kufikia laki moja na elfu ishirini
na tano, baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa vyuo vya elimu ya mafunzo ya
ufundi stadi katika mikoa mine nchini
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt. Shukuru
Kawambwa, amesem Hayo wakati wa ziara ya naibu spika wa Bunge la Korea Kusini
Park Byeong-Seug, ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi
Kwa mujibu wa Waziri Kawambwa, Ujenzi wa
vyuo hivyo umetokana na mkopo wa Dola za Marekani Millioni 8, zaidi ya shilingi
Billioni 10 za Tanzania ilioupata kutoka Serikali ya Korea Kusini
Waziri Kawambwa ameongeza kuwa mara baada
ya kukamilika Ujenzi wake, vyuo hivyo vimefanikiwa kudahili Wanafunzi 1160,sawa
na ongezeko la asilimia 1 ya uwezo wa vyuo vyote nchini. Alisema Waziri
EmoticonEmoticon