NAIBU Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii,
Mhe. Dkt Seif Rashid amekiri kuwepo kwa upungufu wa Vyoo katika Shule za msingi
nchini, na kwamba tayari wanafunzi zaidi ya 450 wamefariki dunia kutokana na
magonjwa ya homa ya matumbo kutokana na vyoo hivyo kuwa vichafu kinyume cha
utaratibu wa kiafya
Akiongea na Waaandishi wa habari leo jijini
Dar es salaam, Naibu waziri huyo amesema kuwa miongoni mwa wagonjwa
wanaohudhuria hosibitali kwaajili ya kupata matibabu ya magonjwa ya Tumbo na
kuhara ni wanafunzi, ambapo kila mwaka ni wanafunzi 45o hufariki dunia kwa
maradhi hayo. Alisema Drkt Seif
“ Hali ya kukosekana kwa vyoo vyenye
mazingira salama kiafya, imesababisha daadhi ya wanafunzi kuugua magonjwa ya
uambukizo yakiwemo magonjwa hatari kama homa ya matumbo, kuhara damu na hata
ugonjwa wa kipindupindu” Alisema Dkt. Seif
Hatahivyo, Asilimia 86 ya shule zilizopo
nchini Tanzania, hazina mazingira na miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu
wa aina mbalimbali ukiwemo wa viungo, kwani ni alisimia 4 tu ya shule nchi
nzima ndio zina niundombinu ya choo kwa watu wenye ulemavu.
“Bado hatuna miundombinu ambayo ni rafiki
kwa watu wenye ulemavu kutokana na asilimia ndogo sana ya shule zetu ndio zenye
miundombinu hiyo, ambayo ni asilimia 4 tu kwa nchi nzima” alisema Dkt. Seif
Mojawapo katiya malengo ya Serikali ndani ya
Sekta ya Elimu, ni kufanikisha matumizi ya Tundu moja la choo kutumiwa na wanafunzi 20 kwa
watoto wakike huku wakiume wakitumia tundu moja wanafunzi 25, mpango ambao
haujafanikiwa hadi hivi sasa. Na kwa mkoa wa Dar es salaam ni shule 6 tu ndizo
zina miundombinu ya choo kwa uwiano wa idadi ya wanafunzi.
EmoticonEmoticon