Wizara ya elimu na
mafunzo ya ufundi nchini Tanzania leo imetoa matokeo ya mtihani wa kidato
cha pili uliofanywa mwaka jana 2012ambapo wanafunzi lakimoja elfu
thelathini na sita 136.000 watalazimika kurudia kidato cha pili, huku
wengine 23 wakifutiwa matokeo yao
Akiongea na
waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Naibu waziri wa Wizara hiyo mheshimiwa Philip
Mulugo amesema
wanafunzi walio feli watalazimika kurudia kidato cha pili, licha ya kiwango cha ufaulu
kupanda kwa asilimia 19.15 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka jana
Waziri amesema,
Serikali imefuta matokeo ya wanafunzi 23 kutokana na vitendo vya
udanganyifu. Waziri ameongeza kuwa kiwango cha ufaulu kwa mikoa ya
kusini yani Lindi na Mtwara ni mabaya kutokana na shule zilizofanya
vibaya kutoka katika mikoa hiyo
Mwaka jana,
wanafunzi wa kidato cha pili walishangaza pale baahi yao walipo chora
Mpira, Mistari ya Muziki na kudanganya katika mitihani yao
EmoticonEmoticon