TIMU
mbili zitakazokamilisha idadi ya timu za kucheza hatua ya Nusu
Fainali ya Kombe la Mapinduzi, zinatarajiwa kujulikana leo, wakati
mechi mbili kali zitakapopigwa kwenye viwanja viwili tofauti visiwani
Zanzibar
Coastal
Union ya Tanga inayoshiriki michuano hii kwa mara ya kwanza,
inamenyana na Miembeni kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung saa 10:30 jioni,
kabla ya mabingwa watetezi Azam FC kupambana na mabingwa wa zamani wa
michuano hii, Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Amaan, kuanzia saa 2:30
usiku wa leo.
Azam
ndio inaongoza Kundi B kwa pointi zake nne, wakifuatiwa na Miembeni
wenye pointi tatu, Coastal pointi mbili na Mtibwa yenye pointi moja
inashika mkia.
Kwa
ujumla, hadi sasa timu yoyote kati ya zote nne za Kundi B inaweza
kufuzu Nusu Fainali na hii inamaanisha hili ndilo lilikuwa Kundi la
kifo.
Kwa
upande wa Kundi A, Hapo jana Simba ilifuzu nusu fainali na kuungana
na Tusker ya Kenya baada ya kutoka Sare ya 1-1 dhidi ya Bandari.
Mabingwa hao wa Tanzania Bara Kikosi cha kwanza kinatarajia kuondoka
nchini kuelekea nchini Oman kwa ajili ya maandali ya mzunguko wa pili
wa ligi na kuacha kikosi cha pili (Simba B) kikiendelea na mashindano
hayo.
Haya
ni mashindano maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 49 ya mapinduzi
Zanzibar sherehe zitakazo fanyika January 12 katika uwanja wa Amaan.
katika soka la kimataifa
Mwanasoka Bora wa Dunia kujulikana leo, kupitia tuzo za (BALLON D'OR) wachezaji ambao wanaupinzani mkubwa katika nafasi hiyo ni Leonel Messi ambaye anachezea Barcelona, Christiano Ronaldo anachezea timu yaReal Madrid na Andre Iniesta ambaye anachezea Barcelona FC
EmoticonEmoticon