Walemavu 150 nchini wamefaidika kwa kupata mikopo midogomidogo,
kwakupitia mfumo wa VICOBA yani Vilage Community Bank, ambayo ilianzishwa mwaka
jana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi ambapo kiasi cha Millioni 100 zilitolewa ilikuwakopesha Walemavu
Akiongea kwenye Hafla iliyo andaliwa kwaajili ya Walemavu Msimamizi
wa Vikoba Bi. Devodha Kitokola ambaye ni Mbunge wa Viti maalum Kupitia chama
cha CCM, alielezea mafanikio ya Mikopo hiyo kuwa,Tayari walemavu 150 wameweza
kukopeshwa, kutoka katika meneo mbalimbali nchini
Aidha Bi. Devodha alisema kuwa Wanategemea kusambaza huduma hiyo
katika vijiji vingi zaidi nchini kwani walemavu niwengi na wote wanaitaji
msaada huwo
"Lengo letu nikuwafikia walemavu wote nchini ilinao waweze
kufaidika kwani tunapokea maombi mengi kutoka seemu nyingi nchini. Alisema Bi
Devodha
Zaidi ya Milioni 100 tayari zimetolewa na Dr. Mengi ilikuendeleza
Vicoba kwa walemavu, kwani walemavu
Wameonyesha juhudi na uwezo mkubwa wakutumia fursa hiyo. Alisema Bi Devodha
Walemavu wengi wameonyesha nia ya kuendeleza kipato chao, na wengi
wao wameahidi kukopa kwa malengo ya baadae ilinawao waje kuwakopesha watu wasio
na ulemavu. Walemavu wameonyesha nia ya kujiendeleza kimapato wao pamoja na
jamii kwa ujumla. Alisema Bi Devodha
EmoticonEmoticon