WASAMARIA WEMA - ANAOMBA MSAADA WENU ILIAPATE FEDHA YA MATIBABU
Mkazi wa Yombo Dovya SALEHE IDDI anaomba msaada wa hali na mali kwa watanzania iliaweze kupata matibabu ya maradhi yanayo msumbua. Bwana Salee anasumbuliwa na tatizo kwenye Ubongo ambao unamsababishia ashindwe kuona vizuri na kutembea.
Bwana Salee amesumbuliwa na hayo maradhi ya ubongo kwa muda wa miaka minne (4 ) sasa. Ameshindwa kuendelea na matibabu kutokana na kukosa fedha ya matibabu. Anamiaka 37 na mke wake amemkimbia kutokana na kuumwa kwa muda mrefu sasa.
"Nimeambiwa Ubongo wangu unamatatizo ya kupokea damu, yani Mishipa aipeleki damu vizuri kwenye Ubongo kitu ambacho kinafanya nakuwa siwezi kufanya kitu chochote pekeyangu" alisema Salehe
Kwa yoyote atakaye penda kumsaidia ampigia kupitia namba zake za mkononi ambayo ni.......
0712 639219 au 0652 357968
Kutoa ni Moyo watanzania wenzangu tumsaidie mwenzetu, ukitaka histori ya ugonjwa wake na matatizo yanayo msibu pamoja na kutoa msaada wako tafadhali piga nomba za hapo juu utampata kwa msaada wako
Hapachini ni vyeti vya matibabu yake ya awali, ila alishindwa kuendelea na matibabu zaidi.
EmoticonEmoticon